الأمم المتحدة: مصر تسير على الطريق الصحيح في إجراءات مواجهة كورونا
Umoja wa Mataifa: Misri iko kwenye njia sahihi kutokana na Hatua za kukabiliana na Corona
قال ريتشارد ديكتس الممثل المقيم للأمم المتحدة فى مصر إن الأمم المتحدة قامت بجمع 2 مليار دولار حتى الأن لمواجهة أزمة فيروس كورونا على مستوى العالم.
Richard Deuts, Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Misri, alisema kuwa Umoja wa Mataifa umekusanya dola bilioni 2 hadi sasa kukabiliana na tatizo la virusi vya Corona ulimwenguni kote.
وأضاف ديكتس فى مداخلة عبر "سكايب" فى برنامج "مساء dmc" أن مصر تسير على الطريق الصحيح في اجراءات مواجهة كورونا، وأن الأمور فى مصر حتى الوقت الراهن جيد، متابعا "لانعلم كم من الوقت نحتاجه للسيطرة على الوباء الحالي على مستوى العالم".
Katika ufuatiliaji kupitia "Skype" kwenye kipindi cha "jioni cha dmc", Dikts aliongezea kwa kusema kwamba Misri iko kwenye njia sahihi kutokana na hatua za kukabiliana na Corona, na kwamba mambo nchini Misri hadi wakati huu ni mazuri,akiendelea "Hatujui ni muda gani tunahitaji kudhibiti juu ya janga la sasa kwa kiwango cha kimataifa."
وأشار إلى أن العديد من الأشخاص على مستوى العالم قد يفقدوا وظائفهم بسبب الأزمة الحالية، وأن اليابان وأمريكا وعدد من الدول بها العديد من الأشخاص الذين خسروا وظائفهم بسبب تداعيات الأزمة الحالية، وشدد على أنه يجب الحفاظ على استمرار اتخاذ الإجراءات الوقائية لمنع انتشار الفيروس، موضحا أن منظمة الصحة العالمية اتخذت العديد من الإجراءات لمواجهة فيروس كورونا المستجد.
Aliashiria kwamba watu wengi ulimwenguni kote huenda wakapoteza kazi zao kwa sababu ya janga liliopo, na kwamba Japan, marekani na nchi kadhaa zina watu wengi ambao wamepoteza kazi zao kwa sababu ya matokeo ya janga liliopo , akasisitiza kwamba muendelezo wa kuchukua hatua za kujikinga lazima zichukuliwe ili kuzuia ueneaji wa virusi hivyo,akifafanua kwamba Shirika la Afya duniani limechukua hatua kadhaa za kukabiliana na virusi vipya vya Corona vinavyoibuka (Covid 19).
ترجمة
أحمد مصطفي متولي
مترجم وباحث متخصص في الشأن الإفريقي