الرئيس الموزمبيقي يتعهد بمواصلة تمكين المرأة
Rais wa Msumbiji anaahidi kuendelea kuwawezesha wanawake
Rais wa Msumbiji, Philip Nyosi, alisema kuwa serikali itaendelea kuweka kipaumbele katika hatua zake ambazo zitaboresha hali ya kijamii ya wanawake, kupitia mikakati na mipango inayotekelezwa na taasisi za umma na za kibinafsi, hii ilikuja wakati wa hutuba ya Nyosi kwa taifa, kutoka Ikulu huko Maputo, kwenye sherehe ya kuadhimisha Siku ya Kitaifa ya Wanawake, ambayo
inaadhimishwa kila mwaka Aprili 7 nchini Msumbiji
وقال الرئيس "ان التزام حكومتنا بزيادة الاستثمار في تعليم الفتيات، من خلال تحسين مؤهلاتهن المهنية من أجل إعادة إدماجهن
بشكل آمن في سوق العمل، يسمح بوجود المزيد من النساء كل عام في مختلف المهن التي تساعد على تطوير البلاد".
"Kujitolea kwa serikali yetu kuongeza uwekezaji katika elimu ya wasichana, kwa kuboresha sifa zao za kitaalamu ili kuwaunganisha tena kwenye soko la ajira, huruhusu kuwepo kwa wanawake wengi kila mwaka katika kazi mbali mbali zinazosaidia kukuza nchi," Rais alisema.
.
Shirika la Televisheni la China la Kimataifa (CGTN) lilimnukuu Nyosi akisema: Wanawake wa Msumbiji wamefanya kazi kubwa katika uundaji wa vizazi vipya, kwa kukuza maadili, amani na haki ya kijamii.
Mbali na maendeleo yaliyofanywa, Rais alikubali kwamba Msumbiji bado ina safari ndefu ili "wanawake wahisi wanalindwa na wanachangia juhudi za pamoja za kukuza nchi", akiongeza kuwa haki za wanawake zinapaswa kukuzwa kwa njia endelevu, akiashiria kuwa moja ya changamoto ni kupambana na unyanyasaji wa nyumbani bila kusita
ترجمة
أحمد مصطفي متولي
مترجم وباحث متخصص في الشأن الإفريقي