شارك السفير أسامة عبد الخالق مندوب مصر الدائم لدي الاتحاد الافريقي ، في أول اجتماع يعقده مجلس السلم والأمن الإفريقي الثلاثاء 14-4-2020، بتقنية الفيديو كونفرنس وتم تخصيصه لمناقشة آثار جائحة الكورونا علي حالة السلم والأمن بإفريقيا.
Balozi Osama Abdel-Khalek, mwakilishi wa kudumu wa Misri kwa Umoja wa Afrika, alishiriki katika mkutano wa kwanza wa Baraza la Amani na Usalama la Afrika Jumanne,Aprili14,2020, kupitia teknolojia ya mkutano wa video, ambao umeandaaliwa kujadili athari za janga la Corona juu ya hali ya amani na usalama barani Afrika.
Katika taarifa hiyo, Abdel-Khalek alionesha juhudi za kitaifa za Misri ili kukabiliana na janga hilo na kulishughulikia, pamoja na ushiriki wake katika uwanja wa ushirikiano wa kimataifa kukabiliana na virusi kupitia kutoa msaada wa matibabu na uhamishaji wa habari na uzoefu.
Mwakilishi huyo wa Misri alitaka Umoja wa Afrika kutekeleza mara moja matokeo ya Ofisi ya Mkutano wa Umoja wa Afrika, ambao Rais alishiriki Machi 28, pamoja na uanzishwaji wa haraka wa Mfuko wa Afrika kukabiliana na Corona kwa njia inayounga mkono uwezo wa kitaifa wa nchi za Kiafrika katika kukuza na kuamirisha afya ya umma, akisisitiza umuhimu wa kwepo kwa mtazamo wa amani, usalama na mageuzi ya uchumi na ulinzi wa kijamii katika njia ya Umoja wa Afrika kukabiliana na janga lililopo.
ترجمة
أحمد مصطفي متولي
مترجم وباحث متخصص في الشأن الإفريقي