الرئيس السيسي يؤكد لرئيس الوزراء الإيطالي تضامن مصر مع روما في محنتها
Raisi Al-Sisi anasisitiza kwa Waziri Mkuu wa Italia, mshikamano wa Misri
pamoja na Roma katika shida yake.
صرح السفير بسام راضي المتحدث الرسمي باسم رئاسة الجمهورية بأن الرئيس عبد الفتاح السيسي أجري الجمعة 3/4 اتصالاً هاتفياً مع رئيس الوزراء الإيطالي جوزيبي كونتي
Balozi Bassam Radi, Msemaji rasmi wa ofisi ya Rais, alisema kwamba Raisi Abdel Fattah Al-Sisi siku ya Ijumaa 3/4 alipigia simu Waziri Mkuu wa Italia Giuseppe Conte.
وصرح المتحدث الرسمي باسم رئاسة الجمهورية بأن الرئيس أعرب مجدداً خلال الاتصال عن خالص التعازي في ضحايا فيروس كورونا المستجد في إيطاليا، مؤكداً سيادته تضامن مصر حكومةً وشعباً مع حكومة وشعب إيطاليا الصديق إزاء انتشار الفيروس، والاستعداد الكامل لتقديم ما يمكن من دعم خلال هذه الظروف الصعبة خاصةً من خلال تبادل الخبرات والتنسيق بين جهات تقديم الرعاية الصحية بالبلدين
Msemaji wa ofisi ya Rais alisema kuwa Rais kwa mara nyingine tena kupitia mawasiliano ya simu alitoa salamu za rambirambi za dhati kwa waathirika wa virusi vya corona nchini Italia, akisisitiza juu ya mshikamano wa serikali na watu wa Misri pamoja na serikali na watu marafiki wa Italia kutokana na kuenea kwa virusi, na utayari kamili wa kutoa msaada unaowezekana wakati wa hali hii ngumu, haswa kupitia kubadilishana uzoefu na uratibu kati ya taasisi zinazotoa huduma ya afya katika nchi hizo mbili
من جانبه أعرب رئيس الوزراء الإيطالي عن خالص تقديره للموقف المصري الداعم لإيطاليا في هذه المحنة، مما يعكس عمق العلاقات التاريخية بين البلدين، مشيراً إلى عزم إيطاليا على تعزيز التعاون المشترك بين السلطات المختصة في البلدين في إطار الجهود الدولية لمكافحة فيروس كورونا المستجد.
Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa Italia alionesha shukrani yake ya dhati kwa msimamo wa misri wa kuunga mkono Italia katika hali hii ngumu, ambayo inaonesha kina cha uhusiano wa kihistoria kati ya nchi hizo mbili, na kuonesha dhamira ya Italia ya kuongeza ushirikiano wa pamoja kati ya mamlaka ya nchi hizo mbili katika mfumo wa juhudi za kimataifa za kupambana na virusi vya Corona vinavyojitokeza covid19
ترجمة
أحمد مصطفي متولي
مترجم وباحث متخصص في الشأن الإفريقي
أحمد مصطفي متولي
مترجم وباحث متخصص في الشأن الإفريقي