موزمبيق: مساعي للحصول على دعم مالي من صندوق النقد والبنك الدولي
Msumbiji: Mipango ya kupata msaada wa kifedha kutoka Mfuko wa Fedha wa Kimataifa na Benki ya Dunia
Serikali ya Msumbiji imepanga kupata misaada ya kifedha kutoka Mfuko wa Fedha la Kimataifa na Benki ya Dunia, Waziri Mkuu alisema anakadiria kuwa nchi hiyo inahitaji dola milioni 700 za Marekani kukabiliana na virusi vya COVID-19.
Tovuti ya ungereza "Born To Invest" iliripoti kuwa Waziri Mkuu wa Msumbiji Carlos Agostino de Rosario alisema kwamba mamlaka hiyo inawasiliana na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa na Benki ya Dunia kuhamasisha rasilimali zinazohitajika na nchi kupambana na janga la COVID-19.
ameongeza, akizungumza wakati wa kuonesha programu ya serikali ya miaka ya 2020 -2024 kwa wabunge." Tunashirikiana" na washirika wetu wa ushirikiano, haswa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa na Benki ya Dunia, kuhamasisha rasilimali,"
De Rosario alionesha kuwa msaada utatumika kuongeza misaada kwa watu masikini zaidi na kupunguza athari za jangala corona katika sekta ya biashara ya kitaifa.
Waziri Mkuu wa Msumbiji alisisitiza juu ya haja ya Msumbiji kusaidia wafanya biashara ndogo ndogo na wa kati katika uwanja wa kutoa dawa, bidhaa na huduma za kimsingi kukabiliana na hali ya dharura iliyosababishwa na COVID-19.
ترجمة
أحمد مصطفي متولي
مترجم وباحث متخصص في الشأن الإفريقي