ضياء رشوان: الرئيس السيسي دائما يتقدم في اللحظة المناسبة ويقف مع شعبه
قال الدكتور ضياء رشوان رئيس الهيئة العامة للاستعلامات ونقيب الصحفيين إن كلمة الرئيس عبدالفتاح السيسي خلال تفقده لعناصر ومعدات القوات المسلحة المخصصة لمواجهة فيروس كورونا تعبر عن معان كثيرة، مشيرًا إلى ذكر الرئيس السيسي لموقف المصريين في ثورة 30 يونيو
Dk. Dia Rashwan, Mwenyekiti wa Mamlaka kuu ya Habari na mwakilishi wa Waandishi wa habari, alisema kwamba hotuba ya Rais Abdel Fattah El-Sisi wakati wa ukaguzi wake wa maafisa na vifaa vya vikosi vya jeshi vilivyoandaaliwa kukabiliana na virusi vipya vya corona, ziara hiyo inaelezea maana nyingi, akiashiria kuwa Rais El-Sisi alitaja msimamo wa Wamisri katika mapinduzi ya Juni 30..
"Rashwan" aliongezea kupitia simu katika kipindi cha "Maoni ya Umma" yaliyotangazwa na Televisheni ya "ten" Jumanne jioni 4/4 kwamba msimamo wa wananchi wa kisiasa katika mapinduzi ya Juni 30 ni sawa na leo, kufuatia: "Rais Al-Sisi kufika katika wakati unaofaa, ili kusimama na watu wanaoteseka Mateso makubwa, kama ilivyotokea Juni 30, lakini kwa maelezo tofauti. "
Alisema kuwa Rais Al-Sisi alizungumzia maswala yote ya watu wa Wamisri, akiongeza kuwa Rais alizungumza juu ya uchumi, mkakati, elimu na afya.
Alishutumu mwenendo wa kampeni kadhaa za kutilia shaka, au kwa vile alivyowaelezea kama kampeni za kupambana na binaadamu, kwa kutumia suala fulani la kuchochea hofu miongoni mwa watu kwa madhumuni ya kisiasa kwa baadhi ya vikundi vinavyopinga serikali, akizungumzia utumiaji fursa wa kikundi cha undugu wa Kiislamu janga la Corona kurudi madarakani hata kwa gharama za maisha ya Wamisri.
Alifafanua kuwa Rais Al-Sisi alisisitiza umuhimu wa kupunguza ajira katika sekta za huduma za serikali. Lakini kwa huduma za uzalishaji, Rais alisisitiza mwendelezo wa kazi, lakini kwa masharti ya kiafya kuhakikisha utunzaji wa usalama wa wafanyikazi, akiashiria ombi la Rais kwa sekta binafsi kufuata utaratibu huu.
ترجمة
أحمد مصطفي متولي
مترجم وباحث متخصص في الشأن الإفريقي