Ghana: IMF( Shirika la fedha duniani) lakubali kutoa dola bilioni moja kwa Ghana ili kupambana na athari za virusi vya corona.Waziri wa Fedha wa Ghana Ken Ovori Atta alisema kuwa imepangiliwa katika wiki hii nchi iweze kupata ufadhili wa haraka uliotolewa na Shirika lafedha la kimataifa kwa kiasi cha dola bilioni moja .
Tovuti ya Ghana "My Joy Online" ilielezea kuwa baraza la utendaji la shirika la fedha la kimataifa lilikuwa limekubali jana Jumatatu juu ya kutoa dola bilioni moja ambazo zitatolewa kwa mujibu wa ufadhili wa haraka, ikiashiria kwamba fedha hizi zitasaidia kukidhi mahitaji ya kifedha, mahitaji ya bajeti ya malipo yanayoikabili Ghana, kuboresha imani nakuhamasisha msaada wa washiriki wengine ya maendeleo. Kama ambavyo itasaidia Ghana katika kudhibiti kuenea Civid-19 na kuunga mkono familia na mashirika yaliyoathirika. Waziri aliongezea kuwa ufadhili utatoa nafasi ya kupanga na itachangia katika utulivu wa uchumi
ترجمة:
أسماء بلال
مترجمة وباحثة متخصصة في الشأن الإفريقي